Machapisho

Picha
kessyngocho.blogspot.com Live:Mwijaku anamjibu Manara muda huu “Manara akasome kwanza” Edwin TZA  ·  1 hour ago NI Mwijaku ambae muda huu anazungumza na Vyombo vya Habari kuhusu kauli za Haji Manara alizozitoka Agosti 4, 2021 akishtumu Uongozi wa Simba SC. “Akubali akatae lazima aende kusoma zama zimebadilika kwasasa mpira unahitaji watu waliosoma, timu zetu zinapoelekea kwasasa zinahitaji watu wenye taaluma kwahiyo asitupie lawama kwa Simba “- Mwijaku Ayo TV iko Mubashara muda huu unaweza ukafuatilia mwanzo mwisho anachozungumza muda huu. MASHABIKI WA SIMBA WAMKINGIA KIFUA MO DEWJI “HATUMTAKI ANAYETOBOA MTUMBWI”  
Picha
kessyngocho.blogspot.com Picha:DC Nikki wa Pili ajipatia chanjo ya Uviko 19 Ni Mkuu wa wilaya ya Kisarawe Nickson Simon maarufu kama  Nikk wa Pili  ambae leo Agosti 5, 2021 amezindua rasmi Chanjo ya kujikinga na Ugonjwa wa Covid-19 katika wilaya yake,  baada ya uzinduzi huo pia  Mkuu  wa  Wilaya  huyo alishiriki kujipatia chanjo hiyo. Baada ya kujipatia chanjo hiyo alisema “ Tunamshukuru Rais Samia na Serikali kwa ujumla pamoja na wadau wote wa afya kwa kufanikisha upatikanaji wa chanjo hii salama kabisa katika nchi yetu. Hii ni hatua muhimu katika kuendeleza mapambano dhidi ya Corona’ – DC Nickson Simon   .   .   MUSUKUMA AWAVAA WANAOSEMA UKICHOMWA CHANJO UNAGEUKA ZOMBIE “NI MANENO YA WAPUMBAVU”
Picha
kessyngocho.blogspot.com Habari kubwa za Magazeti ya Tanzania leo August 1, 2021  Good morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam leo August 1, 2021,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na za nyuma za Magazeti ya Tanzania.
Picha
kessyngocho.blogspot.com Habari za moja kwa moja Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii Habari za moja kwa moja Imepakiwa mnamo 19:18 30 Julai 2021 19:18 30 Julai 2021 Tanzania yapokea ndege ya tisa aina ya Bombardier Ikulu Tanzania Copyright: Ikulu Tanzania Tanzania imepokea ndege nyingine ya masafa ya kati aina ya Bombardier Dash 8- Q 400 kutoka nchini Canada. Ndege hiyo ilipokewa na Rais Samia Suluhu Hassan aliyewaongoza viongozi mbalimbali na baadhi ya watanzania waliojitokeza katika uwanja wa kimataifa wa Julius Nyerere. Hiyo ni ndege ya tisa kati ya 11 zinazotarajiwa kununuliwa na serikali kufikia mwaka 2022, ndege nyingine inatarajiwa kuwasili mwezi Oktoba mwaka huu. Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Dkt Leonard Chamuriho ndege iliyopokelewa leo ni ya 5 ya masafa mafupi kununuliwa na Tanzania tangu mchakato wa kufufua Shirika hilo uanze katika kipindi cha miaka 5 iliyopita. Akizungumza wakati wa kupokea ndege hiyo, Rais wa nchi hiyo, Samia Suluhu alisema mbali na ndege za abiria nchi hiyo...
Picha
kessyngocho.blogspot.com Chanzo kifo cha Babu wa Loliondo “hakutaka wajue anaugua” (+video) Pascal Mwakyoma TZA   Chanzo cha kifo cha Mchungaji Ambilikile Mwasapile (86) kimetajwa aliugua nimonia kali ambayo ilimsababisha kupata tatizo la upumuaji na homa. Tangu afariki wasaidizi wake na majirani wamekuwa wakieleza kushtushwa na kifo hicho ambacho kimetokea akiwa anaendelea kutoa huduma ya tiba ya kikombe aliyoanza tangu mwaka 2011. Mchungaji Ambilikile ambaye ataendelea kukumbukwa kwa kuvutia maelfu ya watu ndani na nje ya nchi kati ya mwaka 2011 hadi 2013 kutokana na tiba yake ya kikombe alifariki jana saa 9:45 jioni. Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro, Raymond Mangwala amesema kuwa taarifa za awali za madaktari zinaeleza chanzo cha kifo ni nimonia ambapo kwa takriban siku tano alikuwa anaumwa na kupata sindano za masaa.
Picha
kessyngocho.blogspot.com PICHA 15:Rais Samia na Viongozi mbalimbali walivyochanjwa chanjo ya Uviko 19 Ikuku DSM Ni July 28, 2021 ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ameshiriki uzinduzi wa chanjo ya Uviko 19 katika viwanja vya Ikulu, Jijini Dar es Salaam. Sasa baada ya uzinduzi huo hapa millardayo.com imekusogezea picha 15 zikimuonesha Rais Samia Suluhu pamoja na Viongozi mbalimbali wakichanjwa chanjo ya kujikinga na Covid-19. . .Rais wa awamu ya sita ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akionesha cheti chake baada ya kupatiwa chanjo ya kujikinga na Covid-19 .Pichani Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akichanjwa chanjo ya kujikinga Covid-19 katika hafla ya uzinduzi wa chanjo hiyo uliofanyika July 28,2021 Ikulu Dar es Salaam . .Pichani:Jaji Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahim Juma akichanjwa chanjo ya kujikinga ugonjwa wa Covid-19 katika uzinduzi wa hafla hiyo uliofanyika July 28,2021 Ikulu Dar es Salaam .Pichani Waziri wa Afya Dkt Dorothy Gw...
Picha
kessyngocho.blogspot.com BOT yapunguza kiwango cha sehemu ya Amana za Mabenki (Video+)   1 hour ago Benki Kuu ya Tanzania  (BOT)  imepunguza kiwango cha sehemu ya Amana za Mabenki kinachotakiwa kuwekwa Benki kuu, hatua hii ni kutoa msukumo mkubwa wa kuongeza kasi ya mikopo kwa sekta binafsi na kupunguza riba na hivyo kuchochea kasi ya ukuaji wa uchumi, hii ni sehemu ya hatua tano za kisera ambazo  BOT  wamezitaja leo ili pia kuweka mambo sawa kutokana na janga la Corona kuathiri shughuli za kiuchumi. Gavana wa Benki Kuu  Prof. Florens Luoga amesema nafuu hii itatolewa kwa  Benki itakayotoa mikopo kwa sekta ya kilimo kulingana na kiasi cha mkopo kitakachotolewa ambapo Benki itakayonufaika itatakiwa kutoa mikopo kwa sekta ya kilimo kwa riba isiyozidi asilimia 10 kwa mwaka. Hatua nyingine ambayo imechukuliwa na BOT ni pamoja na kulegeza masharti ya usajili wa  Mawakala  wa Benki ambapo imeondoa sharti la uzoefu wa kufanya biashara kwa angalau mi...