Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Juni 20, 2021

Na hii ndo sababu ya vyama vya ushirika vimekua mzigo

Picha
Waziri wa kilimo, Husein Bashe ameviagiza vyama vya ushirika nchini kutumia vizuri mikopo inayokopa kutoka kwenye mabenki mbalimbali ili ilete tija kwa wakulima wanachama badala kuitumia mikopo hiyo kwenye shughuli za uendeshaji wa miradi isiyo na tija kwa wanachama hao. Bashe alitoa agizo hilo wakati akifunga Mkutano Mkuu wa wadau wa Kahawa uliofanyika mwishoni mwa wiki jiji Dodoma ukihudhuliwa na wadau mbalimbali wakiwemo wakuu wa mikoa na wilaya zinazolima kahawa, wakulima na taasisi zinazoshughulika na kilimo hicho pamoja na wafanyabiashara. Alibainisha kuwa kwasasa baadhi ya vyama hivyo vinapitia wakati mgumu na kukosa tija kwa wakulima kwa kuwa vimeandamwa na madeni kutoka kwa baadhi ya benki, madeni ambayo kimsingi yametokana na matumizi yasiyo na tija kwa vyama hivyo bila kuwashirikisha wanachama. “Na hii ndio sababu vyama vya ushirika vimekuwa mzigo kwa wakulima ambao kwa sasa wanalazimika kubeba mzigo wa kulipa madeni ambayo hawajahusika kuyatengeneza. ’’ alisema Bashe ambae ...