Na hii ndo sababu ya vyama vya ushirika vimekua mzigo

Waziri wa kilimo, Husein Bashe ameviagiza vyama vya ushirika nchini kutumia vizuri mikopo inayokopa kutoka kwenye mabenki mbalimbali ili ilete tija kwa wakulima wanachama badala kuitumia mikopo hiyo kwenye shughuli za uendeshaji wa miradi isiyo na tija kwa wanachama hao.

Bashe alitoa agizo hilo wakati akifunga Mkutano Mkuu wa wadau wa Kahawa uliofanyika mwishoni mwa wiki jiji Dodoma ukihudhuliwa na wadau mbalimbali wakiwemo wakuu wa mikoa na wilaya zinazolima kahawa, wakulima na taasisi zinazoshughulika na kilimo hicho pamoja na wafanyabiashara.

Alibainisha kuwa kwasasa baadhi ya vyama hivyo vinapitia wakati mgumu na kukosa tija kwa wakulima kwa kuwa vimeandamwa na madeni kutoka kwa baadhi ya benki, madeni ambayo kimsingi yametokana na matumizi yasiyo na tija kwa vyama hivyo bila kuwashirikisha wanachama.

“Na hii ndio sababu vyama vya ushirika vimekuwa mzigo kwa wakulima ambao kwa sasa wanalazimika kubeba mzigo wa kulipa madeni ambayo hawajahusika kuyatengeneza. ’’ alisema Bashe ambae pia alitaka vyama hivyo kuanzia mwakani vianze kuwanufaisha wakulima  badala ya kuendelea kuwekeza fedha kwenye miradi isiyo na tija” Bashe

“Mnajua haiingii akilini kabisa kuona kwamba vyama vya ushirika vinatengeneza mabilioni kupitia makato ya wakulima lakini vinashindwa kuwasaidia pale wanapokuwa na changamoto mbalimbali ikiwemo hata zile muhimu za kifamilia. Fedha zote zinaenda kulipa madeni ambayo kimsingi yamezalishwa na viongozi wanaoongoza vyama hivi kwa maslahi yao binafsi…naomba hili lifike mwisho sasa.’’ Bashe

Akizungumzia changamoto ya matumizi mabaya ya mikopo kwenye vyama vya ushirika, Meneja wa benki ya NBC tawi la Dodoma Happiness Kizigira alisema ili kukabiliana na changamoto hiyo, benki hiyo imekuwa na utaratibu wa kuendesha mafunzo kuhusu namna bora ya kutumia mikopo kabla ya kuwapatia walengwa hatua ambayo imesaidia sana kupunguza tatizo hilo.

“Pamoja na mambo mengine lengo la mikopo yetu huwa kuhakikisha tunamsaidia mlengwa kukuza mtaji wake na kufanya shughuli zake kwa ufanisi na ushindani ili atengeneze faida itakayomuwezesha kurejesha fedha kwetu bila changamoto. Hili kufanikisha hili wateja weteja wetu zikiwemo AMCOS wamekuwa wakipata mafunzo ya namna bora ya kuendesha shughuli zao kutoka kwa wataalam tunaoshirikiana nao…hii imesaidia sana!’’ alitaja.


Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

DARAJANI TANZANITE DAR ESALAAM