Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Septemba 24, 2021

NAKUKARIBISHA UTAZAME KILICHO ANDIKWA NYUMA NA MBELE KWENYE MAGAZETI YA LEO TRH 25/09/2021

Picha
kessyngocho.blogspot.com Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam leo September /25/ 2021 nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na za nyuma za Magazeti ya Tanzania.

BUNGE LAJADILI UJERUMANI KULIPA FIDIA MAUAJI YA KIMBARI

Picha
kessyngocho.blogspot.com Bunge nchini Namibia litajadili makubaliano kati ya nchi hiyo na Ujerumani katika hatua ya kulipa fidia ya wahanga wa mauaji ya kimbari yaliyofanyika kipindi cha ukoloni wa kijerumani ambayo bado hayajasainiwa hadi kufikia sasa,Majadiliano ya bunge nchini Namibia kuhusu makubaliano kati ya nchi hizo yanatarajiwa kuanza tena Jumatano mwezi huu. Spika wa Bunge nchini Namibia, David Nahongandja amesema ana matumaini makubwa katika makubaliano hayo na hatua hiyo itapelekea kupigiwa kura siku zijazo kwa kuwa,Kura hiyo ilicheleweshwa baada ya vikao vya bunge kuahirishwa mwezi Juni kutokana na kuongezeka kwa maambukizi ya virusi vya corona. Kwa mujibu wa Nahongandja, wabunge wa upinzani mara kwa mara waliizuia serikali kuwasilisha makubaliano hayo bungeni hapo kwa siku ya jana,na kupelekea zaidi ya watu 300 waliandamana nje ya jengo la bunge kupinga makubaliano yaliyopendekezwa.