Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Julai 22, 2021
Picha
kessyngocho.blogspot.com Treni yapata ajali Morogoro ikiwa na abiria 1370 ‘Dereva amefariki, kuna Majeruhi’ Shirika la Reli Tanzania  (TRC)  limesema Treli ya  Abiria  imepata ajali saa tatu asubuhi July 22, 2021  baada ya  Lori  kuigonga Treni hiyo katika eneo la Kambi moa Godegode, Morogoro  na kupelekea  majeruhi 21  ambapo Wanaume ni  13  na Wanawake  8  na kifo cha Dereva wa Lori ambaye jina lake ni  Gerald Malandu. Treni hiyo iliyokuwa ikitokea  Dodoma kuelekea Dar es salaam ilikuwa na abiria 1370  na tayari majeruhi wamefikishwa Zahanati ya  SGR  Kidete kwa  Matibabu
Picha
kessyngocho.blogspot.com Tony Blair akutana na Rais Samia “Taasisi yake ipo tayari kusaidia chanjo” (+picha) Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, leo tarehe 22 Julai, 2021 amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu Mstaafu wa Uingereza Mhe. Tony Blair, Ikulu Jijini Dar es Salaam. Tony Blair ambaye ni Mwenyekiti Mtendaji wa Taasisi ya Mabadiliko Ulimwenguni ( Tony Blair Institute for Global Change ) amemhakikishia Rais Samia kuwa taasisi yake inaunga mkono jitahada mbalimbali anazochukua katika kuwaletea maendeleo wananchi wa Tanzania. Amesema taasisi yake inafanya kazi katika nchi 16 Afrika ikijikita kutekeleza vipaumbele vya Serikali zao ambapo amsema katika kipindi cha mwaka mmoja na nusu taasisi yake imejikita zaidi katika masuala ya kukabiliana na janga la UVIKO 19.