Tanzania
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kesho Ijumaa May 7, 2021 anatarajia kuzungumza na wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam katika mkutano utakaofanyika ukumbi wa Mlimani City na kuhusisha wazee takribani 900. Hayo yameelezwa leo Mkuu wa Mkoa wa DSM, Abubakar Kunenge aliyebainisha kuwa kulikuwa na utaratibu maalum wa kuwapata wazee hao na kwamba wengine wanapaswa kufuatilia mkutano huo kupitia vyombo mbalimbali vya habari. “Tunaomba sana waliopata mwaliko wahudhurie mkutano huu, tunatarajia ikifika saa nane kamili wazee wote watakuwa wameshafika. Na utaratibu wa jinsi ya kufika utatolewa kwani kutakuwa na magari yameandaliwa.” Kunenge “Tunamshukuru Rais kwa kuchagua Mkoa huu kwa sababu angeenda Mkoa wowote lakini amechagua Dar es Salaam. Ninaamini kuongea na wazee hao atakuwa ameongea na wazee wa Tanzania nzima,” Kunenge