Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Agosti 18, 2021
Picha
kessyngocho.blogspot.com Chanjo ya Ukimwi yaanza kufanyiwa Majaribio Edwin TZA  ·  24 minutes ago Wakati chanjo ya corona ikiendelea kutolewa katika Mataifa mbalimbali Duniani, chanjo ya Virusi vya  UKIMWI  (VVU) iliyokuwa inafanyiwa utafiti muda mrefu na Kampuni ya Moderna ya Marekani inatarajiwa kuanza kufanyiwa majaribio kwa Binadamu leo  Jumatano . Kampuni hiyo imetengeneza chanjo za aina mbili za  UKIMWI  ambazo zimefuzu hatua za awali za kimajaribio na hivyo kuanza kutumika kwa binadamu katika awamu ya tatu, chanjo hizo ni  mRNA-1644 na mRNA-1644v2-Core  ambazo zimeshachunguzwa na kufanyiwa majaribio ya awali na kuonekana salama kabla ya kujaribiwa kwa Binadamu kwa mara ya kwanza. Chanjo hiyo itaanza kutolewa kwa Watu  56 wenye umri wa kati ya miaka  18 hadi 56  na majaribio yanatarajiwa kukamilika Mwaka 2023.
Picha
kessyngocho.blogspot.com PICHA 10:Mwenge ulivyokabidhiwa DSM, Wakuu wa Wilaya washuhudia Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Amos Makalla leo August 18 amepokea Mwenge wa Uhuru uliowasili Asubuhi ya leo Uwanja wa ndege wa  Mwalimu Nyerere  ukitokea Mkoa wa Pwani na kuukabidhi kwa Wilaya ya Ilala kwaajili ya kuanza shughuli ya uzinduzi na uwekaji mawe ya msingi kwenye miradi ya miradi ya maendeleo. Akipokea Mwenge huo kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe. Aboubakar Kunenge,  RC Makalla  amesema kwa siku tano ambazo Mwenge wa Uhuru utakuwa  Dar es salaam  utapitia miradi ya maendeleo 46 yenye thamani ya Shillingi  Billion 105.1. Mwenge wa Uhuru umeanza rasmi kukimbizwa leo Mkoa wa  Dar es salaam  kwa kuanzia Wilaya ya Ilala Kisha  Ubungo, Kinondoni, Kigamboni na Temeke   ambapo ifikapo August 23 Mwenge huo utakabidhiwa kwa Mkoa wa Lindi ukienda na kaulimbiu inayolenga kuhimiza Matumizi sahihi ya  TEHAMA . . . . . . . . .