Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Septemba 23, 2021

MAHAKAMA KUU IMEFUTILIA MBALI KESI YA MBOWE

Picha
kessyngocho.blogspot.com Mahakama Kuu imefutilia mbali kesi ya Mbowe Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya  Dar es  Salaam  imetupilia mbali kesi ya kikatiba ya Mwenyekiti wa CHADEMA,  Freeman Mbowe  aliyokuwa akilalamika kwamba haki zake za kikatiba zilikiukwa wakati wa kumkamata, kumweka kizuizini na hatimaye kumfungulia kesi akikabiliwa na mashtaka ya ugaidi. Mahakama  hiyo ilifikia uamuzi huo mbele ya Jaji John Mgeta baada ya kukubaliana na hoja moja kati ya tatu za  Serikali  ya pingamizi la awali kuwa maombi hayo hayako sawa kisheria kwasababu yanapingana na kifungu  4(5)  na kifungu cha  8(2)  cha sheria ya haki za msingi na utekelezaji wa majukumu sura ya tatu. Kwamba Mbowe ana njia nyingine za kupata hayo anayo walalamikia. Jaji alisema, wakati maombi hayo yameletwa, wakati huo huo kuna mwenendo wa kesi katika Mahakama nyingine ambako Mbowe anashtakiwa kesi ambayo ndiyo msingi wa malalamiko ha...