Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Juni, 2021
Rais Samia Suluhu Hassan amesema serikali itavilipa vyombo vya habari deni la zaidi ya Sh6 bilioni baada ya kufanya uhakiki wa deni hilo ambalo ni moja ya mambo yaliyosababisha kufa kwa baadhi ya vyombo hivyo. Rais Samia ametoa ahadi hiyo  jijini Dar es Salaam wakati akijibu swali la mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Deodatus Balile aliyemuomba kiongozi mkuu huyo wa nchi kutimiza ahadi iliyotolewa na Waziri Mkuu, Kassimu Majaliwa ya kulipa deni hilo kabla ya Juni 30, 2021. Amesema Serikali itafanya uhakiki wa madeni hayo ya vyombo vya habari, kIsha itaanza kulipa kidogokidogo mpaka deni hilo liishe. “Nitafanya kazi na waziri mkuu katika kuhakikisha kwamba tunalipa madeni haya kidogokidogo lakini lazima tuyafanyie uhakiki kisha tuweze kulipa, hatutaweza kulipa kwa mkupuo,”  Rais Samia Kuhusu katazo la Serikali kutangaza kwenye vyombo vya habari, Rais Samia amesema tangu ameingia ofisini, hajaona kama kulikuwa kuna katazo hilo hata hivyo katika utawala wake hakutakuwa  na
Picha
 TZA  ·  Yesterday Kuelekea kilele cha Maadhimisho ya Siku Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Juni 26 ya kila mwaka imesema serikali haina mpango wa kuruhusu kilimo cha bangi na kama ikiruhusu ni Taasisi za Utafiti zitaruhusiwa. Akizungumza na waaandishi wa habari  Gerald Musabila Kusaya  Kamishna wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za kulevya amesema mpaka sasa Serikali haina mpango wowote wa kuruhusu kilimo hicho .

Na hii ndo sababu ya vyama vya ushirika vimekua mzigo

Picha
Waziri wa kilimo, Husein Bashe ameviagiza vyama vya ushirika nchini kutumia vizuri mikopo inayokopa kutoka kwenye mabenki mbalimbali ili ilete tija kwa wakulima wanachama badala kuitumia mikopo hiyo kwenye shughuli za uendeshaji wa miradi isiyo na tija kwa wanachama hao. Bashe alitoa agizo hilo wakati akifunga Mkutano Mkuu wa wadau wa Kahawa uliofanyika mwishoni mwa wiki jiji Dodoma ukihudhuliwa na wadau mbalimbali wakiwemo wakuu wa mikoa na wilaya zinazolima kahawa, wakulima na taasisi zinazoshughulika na kilimo hicho pamoja na wafanyabiashara. Alibainisha kuwa kwasasa baadhi ya vyama hivyo vinapitia wakati mgumu na kukosa tija kwa wakulima kwa kuwa vimeandamwa na madeni kutoka kwa baadhi ya benki, madeni ambayo kimsingi yametokana na matumizi yasiyo na tija kwa vyama hivyo bila kuwashirikisha wanachama. “Na hii ndio sababu vyama vya ushirika vimekuwa mzigo kwa wakulima ambao kwa sasa wanalazimika kubeba mzigo wa kulipa madeni ambayo hawajahusika kuyatengeneza. ’’ alisema Bashe ambae

Habari kutoka millardayo

Sharifat Hytham  ni mtoto wa Kitanzania mwenye  miaka 8  akiwa anasoma  Darasa la 4 katika Shule ya  Yemen  Dar es Salaam.  Ayo TV na Millardayo.com  imekutana na Sharifati ambae ana uwezo wa hali ya juu unaowashangaza wengi ikiwemo kuwaombea watu Dua, kuwafundisha Wanafunzi wenzake waliomzidi umri na kidato.   ‘ Naitwa Sharifat Hytham nasoma katika shule ya Yemen Primary, mimi ni mtoto wa kwanza katika familia yetu upande wa Mama na nina mdogo wangu wa kiume, muda ninaopata kusoma ni muda wa kukaa pekee yangu jioni tulivu pia nina muda wa kuwafundisha wenzangu kwa kipawa nilichopewa  na Mwenyezi  Mungu amenipa wepesi na amenijaalia wa kuwafundisha wenzangu walionivuka Madarasa na kiumri’- Sharifat Hytham

Habari za watu wazima tanzania

Kama kuna mtu anahabari za ukweli atupe tuwe tunatuma kwenye blog yetu hii