Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Julai 27, 2021
Picha
kessyngocho.blogspot.com BOT yapunguza kiwango cha sehemu ya Amana za Mabenki (Video+)   1 hour ago Benki Kuu ya Tanzania  (BOT)  imepunguza kiwango cha sehemu ya Amana za Mabenki kinachotakiwa kuwekwa Benki kuu, hatua hii ni kutoa msukumo mkubwa wa kuongeza kasi ya mikopo kwa sekta binafsi na kupunguza riba na hivyo kuchochea kasi ya ukuaji wa uchumi, hii ni sehemu ya hatua tano za kisera ambazo  BOT  wamezitaja leo ili pia kuweka mambo sawa kutokana na janga la Corona kuathiri shughuli za kiuchumi. Gavana wa Benki Kuu  Prof. Florens Luoga amesema nafuu hii itatolewa kwa  Benki itakayotoa mikopo kwa sekta ya kilimo kulingana na kiasi cha mkopo kitakachotolewa ambapo Benki itakayonufaika itatakiwa kutoa mikopo kwa sekta ya kilimo kwa riba isiyozidi asilimia 10 kwa mwaka. Hatua nyingine ambayo imechukuliwa na BOT ni pamoja na kulegeza masharti ya usajili wa  Mawakala  wa Benki ambapo imeondoa sharti la uzoefu wa kufanya biashara kwa angalau miezi 18 kwa Waombaji wa biashara ya Wakala wa

Ngorongoro

Picha
kessyngocho.blogspot.com Hifadhi ya Ngorongoro   (kwa   Kiingereza : "Ngorongoro Conservation Area") ni   hifadhi ya taifa   kaskazini mwa   Tanzania   inayojulikana kote   duniani , hasa baada ya kuorodheshwa na   UNESCO   kati ya mahali pa   Urithi wa Dunia . Makundi ya wanyamapori katika kasoko. Ramani ya eneo. Eneo la Ngorongoro lipo kaskazini mwa Tanzania. Ndani ya kasoko. Kiini chake ni eneo la  kasoko  kubwa lenye  umbali  wa takriban  kilomita  180 kutoka  Arusha . Kuna jumla ya  wanyamapori  wakubwa takriban 25,000, wakiwa pamoja na  vifaru ,  viboko ,  nyumbu ,  pundamilia ,  nyati ,  simba ,  fisi  na  chui . Bidii kubwa zaidi ya kulinda wanyama aina ya vifaru zinahitajika haraka kwa sababu idadi ya wanyama hao inazidi kupungua. Mabaki ya  zamadamu  katika  Olduvai Gorge yanaonyesha kwamba  wanyama  hao waliokoma walikuweko tangu miaka  milioni  3 iliyopita. Mwaka   1979  Ngorongoro ilipokewa katika orodha ya  Urithi wa Dunia  ya  UNESCO  upande wa  uasilia . Katik
Picha
kessyngocho.blogspot.com Rais Samia akiwaapisha Mabalozi wateule 13 “Tumeteuwa Vijana ili mkachape kazi” Edwin TZA  ·  2 hours ago NI July 27, 2021 ambapo Rais wa awamu ya sita ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , Samia Suluhu Hassan  anawaapisha Mabalozi wateule 13 muda huu Ikulu Dar es Salaam “Waziri amesema hapa ni uteuzi wa Vijana wenye umri wa chini ya miaka 45 sasa hii ina maana gani? hii ina maana kwamba hatujawapa Idara mkafanye ujana tumteuwa vijana tuna maana kwamba ulimwengu wa leo ni ulimwengu wa mitandao, taarifa nyingi ni mitandao, mawasiliano mingi ni mitandao na nyie vijana mpo wepesi kwenye hayo” – Rais Samia “ Lakini pia mtakuwa wepesi kufuatilia yanayowahusu lakini pia kufanya kazi zenu kwa urahisi tuna imani na nyinyi lakini pia kwa ambao watabaki hapa ndani watafanya kazi zao kwa urahisi, t umechagua fani mbalimbali tukijua kwamba fani zenu zikienda kutusaidia ikiwemo  wafanyabiashara watu wa Dipolamasia nikijua kwamba kazi iliyopo mbele yenu mnaiweza’-  Rais Samia

Mzozo eneo la karume

Picha
kessyngocho.blogspot.com Mzozo eneo la Karume, Serikali ya Zanzibar yatoa kauli (Video+) Edwin TZA  ·  3 hours ago Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema uwepo wa Chuo cha kumbukumbu ya Mwalimu  Nyerere visiwani Zanzibar  ni kielelezo Chanya katika kuenzi na kudumisha Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kwa Vitendo. Makamu wa Pili wa Rais  wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla ameleza hayo kupitia hotuba alioisoma kwa niaba ya Rais Dk. Hussein Mwinyi  katika hafla ya uwekaji wa Jiwe la Msingi la mradi wa ujenzi wa mabweni ya wanafunzi  wa chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere – Kampasi ya Karume Zanzibar. ‘Suala la mzozo Mkuu wa chuo amelizungumza na mimi nilitaka kumuhakikishia kwamba kwa niaba ya Mheshimiwa Rais hili suala tutalimaliza kwa kipindi kijazo’- Makamu wa Pili wa rais wa Zanzibar  

Mkuu wa wilaya saimon songwe simalenga

Picha
kessyngocho.blogspot.com Mkuu wa Wilaya ya Songwe,  Saimon Simalenga  amepiga marufuku makongamano na mikusanyiko isiyo ya lazima ndani ya  Wilaya  hiyo kwa lengo la kuwakinga Wananchi na maambukizi ya Virusi vya Corona.  Simalenga  ametoa katazo hilo jana wakati akizungumza na Wandishi wa Habari Wilayani  Songwe. Hata hivyo, Simalenga amesema marufuku hiyo haiwahusu waumini wa dini zote ambao wanaruhusiwa kuendelea kufanya ibada kama Kawaida, lakini akiwataka wachukue tahadhari dhidi ya virusi vya  Corona wanapokuwa ibadani. “Kuanzia sasa hakuna mikusanyiko isiyokuwa ya lazima itaruhusiwa kufanyika ndani ya Wilaya ya Songwe, tunazuia mikusanyiko hivyo kwa nia njema ya kuzuia kusambaa kwa maambukizi ya virus vya Corona,”  alisema Simalenga. Simalenga amesema kila atakayetaka kufanya kongamano lolote lazima awasiliane na ofisi ya Mkuu wa Wilaya kabla hajafanya ili apewe kibali kwa kuzingatia mazingira yaliyopo na kama  Serikali  itajiridhisha kuwa msongamano huo hautakiwa na athari za k