Ushauri
Karibu rafiki yangu mpendwa kwenye makala ya ushauri wa changamoto, ambapo tunashauriana hatua sahihi za kuchukua katika kukabiliana na changamoto ambazo ni kikwazo kwetu kufanikiwa kimaisha. Moja ya changamoto ambayo wengi wanapitia ni kukwama kuanza kwa sababu ya kuamini bado hawajapata maarifa ya kutosha au hakuna wa kuwasaidia. Hilo linawapelekea kujikuta wanaendelea kujifunza na kusubiri na wasianze kabisa. Kwenye ushauri wa leo tunakwenda kuona jinsi unavyojizuia kuanza kwa kufikiri hujawa na elimu ya kutosha au hatuna watu wa kutusaidia. Na rafiki yetu John ametuandikia kuomba ushauri kwenye hili; “Ninatamani kufanya biashara lakini kila ninayetaka kuzungumza naye na kushirikiana naye hasaidii kufika kwenye lengo langu kuhusu biashara na ninajikuta nabaki na maarifa yangu. Pia nimefanya tafiti nyingi kuhusu biashara na kilimo lakini kinachonikwamisha ni kukosa msingi bora wa elimu na kukosa mtu atakaye kusaidia kufikia malengo je nifanyeje. – John E. M. Nakumbuka kwenye moj...