Habari kutoka millardayo
Sharifat Hytham ni mtoto wa Kitanzania mwenye miaka 8 akiwa anasoma Darasa la 4 katika Shule ya Yemen Dar es Salaam. Ayo TV na Millardayo.com imekutana na Sharifati ambae ana uwezo wa hali ya juu unaowashangaza wengi ikiwemo kuwaombea watu Dua, kuwafundisha Wanafunzi wenzake waliomzidi umri na kidato. ‘ Naitwa Sharifat Hytham nasoma katika shule ya Yemen Primary, mimi ni mtoto wa kwanza katika familia yetu upande wa Mama na nina mdogo wangu wa kiume, muda ninaopata kusoma ni muda wa kukaa pekee yangu jioni tulivu pia nina muda wa kuwafundisha wenzangu kwa kipawa nilichopewa na Mwenyezi Mungu amenipa wepesi na amenijaalia wa kuwafundisha wenzangu walionivuka Madarasa na kiumri’- Sharifat Hytham