Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Agosti 17, 2021
Picha
kessyngocho.blogspot.com Tambo za Dulla Mbabe kuelekea Pambano lake na Twaha Kiduku “Yule sio Bondia” Edwin TZA  ·  26 minutes ago Ni kutoka kwenye kambi ya Bondia  Dulla Mbabe  ambaye amefunguka maandalizi ya pambano lake na Bondia Twaha Kiduku ambalo linatarajiwa kufanyika  Ijumaa  hii katika Ukumbi wa Ubungo Plaza Dar es Salaam. Bondia huyo akizungumza na Ayo TV & Millardayo.com alisema. ..”Nimeshajiandaa muda tu tumalize mzizi wa fitina , kwanza lazima crown ibaki katika mkoa wa Dar halafu ndipo itaenda Pwani Kisarawe”- Dulla Mbabe Bonyeza Play kufahamu alichozungumza Dulla Mbabe  kuhusu Pambano lake dhidi ya Twaha Kiduku
Picha
kessyngocho.blogspot.com Waziri amvaa vikali Askofu Gwajima “Ananivurugia Wizara, majeshi yote akamatwe” (Video+) Edwin TZA  ·  2 hours ago Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto  Dr. Doroth Gwajima ameliagiza Jeshi la Polisi na Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa  ( TAKUKURU)  kumkamata na kumhoji Mbunge wa Kawe Askofu  Josephat Gwajima  ili athibitishe kauli anazozitoa dhidi ya Serikali na Viongozi kuhusu chanjo ya  Covid-19. Dr. Gwajima ametoa agizo hilo leo Jumanne  Agosti 17, 2021  katika kijiji cha Kyatunge Butiama na kusema  Askofu Gwajima amekuwa akitoa taarifa za kupotosha kwa makusudi jambo linaloivuruga Wizara yake na Serikali katika mapambano dhidi ya ugonjwa huo. “Gwajima ni ndugu yangu, ni shemeji yangu kabisa, lakini mimi ni waziri nimekula kiapo cha kutumikia nchi yangu sio kumtumikia shemeji yangu. Mimi ndiye msemaji wa masuala ya afya nchini, nimechoka kuvuruguwa, naagiza Majeshi yote Polisi, TAKUKURU akamatwe popote alipo ahojiwe juu ya haya
Picha
kessyngocho.blogspot.com Watalii 250 waingia Tanzania “tahadhari imechukuliwa juu ya Uviko-19 Mamia ya Watalii kutoka Israel waendelea kuja nchini kutembelea vivutio mbalimbali vya utalii licha ya changamoto ya Ugonjwa wa UVIKO-19 ambao umeikumba dunia hivi sasa. Kuja kwa watalii hao kunatokana na sio tu Tanzania kubarikiwa kuwa na vivutio vingi vya utalii, bali pia hatua za tahadhari zinachokuliwa na Serikali dhidi ya maambukizi ya virusi vya UVIKO-19. Hatua hizo ambazo zimewejengea imani watalii kuendelea kuja nchini zimetambuliwa na Baraza la Wasafiri na Utalii Duniani (World Travels and Tourism Council-WTTC) ambapo Mwezi Agosti 2020 baraza hilo liliitangaza Tanzania kuwa nchi salama ya kuitembelea. Akizungumza Jijini Arusha, wakati wa hafla ya kuwapokea watalii takribani 100 kutoka Israel na wengine 150 waliokuwa wanaagwa, Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,  Balozi Hemedi Mgaza  amesema ujio wa watalii hao umet