Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dr. Doroth Gwajimaameliagiza Jeshi la Polisi na Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa ( TAKUKURU) kumkamata na kumhoji Mbunge wa Kawe Askofu Josephat Gwajima ili athibitishe kauli anazozitoa dhidi ya Serikali na Viongozi kuhusu chanjo ya Covid-19.
Dr. Gwajima ametoa agizo hilo leo Jumanne Agosti 17, 2021 katika kijiji cha Kyatunge Butiama na kusema Askofu Gwajimaamekuwa akitoa taarifa za kupotosha kwa makusudi jambo linaloivuruga Wizara yake na Serikali katika mapambano dhidi ya ugonjwa huo.
“Gwajima ni ndugu yangu, ni shemeji yangu kabisa, lakini mimi ni waziri nimekula kiapo cha kutumikia nchi yangu sio kumtumikia shemeji yangu. Mimi ndiye msemaji wa masuala ya afya nchini, nimechoka kuvuruguwa, naagiza Majeshi yote Polisi, TAKUKURU akamatwe popote alipo ahojiwe juu ya haya madai yake na hatua zichukuliwe” Waziri Gwajima
“ASKOFU GWAJIMA AKAMATWE, AHOJIWE ANAPOTOSHA” WAZIRI GWAJIMA
Maoni
Chapisha Maoni
Karibu kessyngocho.blogspot.com
Tukuhudumie