WATOTO WAWILI WAFARIKI KWA KUKOSA HEWA

kessyngocho.blogspot.com

Watoto wawili wa familia moja wenye umri wa mwaka mmoja na mwingine wa mmoja na nusu wamefariki dunia baada ya kukosa hewa ya kutosha kwasababu ya uwepo wa jiko la moto ndani ya nyumba waliyokuwa wamelala na wazazi wao kwa lengo la kujikinga na baridi huko katika Kijiji cha Usuhilo Manispaa ya Tabora.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, ACP Richard Abwao amekiri kutokea kwa tukio hilo la kuhuzunisha nyumbani kwa Athuman Shaban huku akiwataja watoto waliofariki kuwa ni Aman Athuman mwaka mmoaja na nusu (1.6) na Zainab Athuman aliyekuwa na mwaka mmoja (1).

Chanzo cha kifo hicho ni jiko la moto lililokuwa limewekwa ndani ili kusaidia kujikinga na baridi walipokuwa wamelala ndani na wazazi wao ambapo katika tukio hilo watu watatu bado hali zao siyo nzuri na wamelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tabora Kitete huku watoto wawili waliofariki tayari wameshazikwa huko Kijiji cha Usuhilo.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

DARAJANI TANZANITE DAR ESALAAM