Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia 2021
Picha
kessyngocho.blogspot.com LIVE: Rais Samia anahutubia Taifa usiku huu Muda huu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan anahutubia Taifa kuelekea miaka 60 ya Uhuru, bonyeza PLAY hapa chini kutazama LIVE
Picha
kessyngocho.blogspot.com Mkurugenzi wa gereza ahukumiwa miaka mitano Mahakama ya Rwanda imemuhukumu kifungo cha miaka mitano jela aliyekuwa Mkurugenzi wa Gereza kuu la Kigali kwa kosa la kuiba pesa za mfungwa wa Uingereza. Innocent Kayumba, ambaye alihukumiwa Ijumaa jioni pamoja na makamu wake wa zamani Eric Ntakirutimana, amekata rufaa dhidi ya hukumu hiyo, hati ya mahakama inaonyesha. Mahakama ilimwachilia mfungwa mtaalamu wa IT ambaye alitumia ujuzi wake kudukua kadi ya Visa ya mwathiriwa baada ya kuiambia mahakama kwamba alilazimishwa na mkurugenzi wa gereza kufanya hivyo. Alisema alitakiwa “kuichambua” kadi iliyohifadhiwa na uongozi wa magereza baada ya kubaini kuwa akaunti ya benki iliyounganishwa nayo ilikuwa na kiasi kikubwa cha fedha. Mfungwa huyo mwenye uraia wa Uingereza na Misri aliiambia mahakama kwamba zaidi ya £7,000 ($9,300) zilichukuliwa kutoka kwa akaunti yake kwa kutumia kadi yake mwaka jana bila yeye kujua. Mahakama ilisema Kayumba na naibu wake walipanga njama ya w
Picha
kessyngocho.blogspot.com Mikopo kwa watakaofunga ndoa Mgombea urais nchini Kenya ameahidi mikopo ya kati ya $4,400 (£3,300) na $8,800 kwa wanandoa wote wapya iwapo atachaguliwa kuwa Rais katika uchaguzi utakaofanyika mwakani. Gavana wa Machakos Alfred Mutua, ambaye alikuwa akizindua ilani yake ya urais Jumapili, alisema mkopo wa riba ya chini utakaolipwa ndani ya miaka 20 utasaidia familia “kuanza maisha vizuri”. Vilevile mgombea huyo amesema serikali yake itahimiza upandaji miti na kuhesabiwa kama sehemu ya malipo ya mahari. “Unapoenda kulipa mahari, unapaswa kusema umepanda miti mingapi,” Bw. Mutua alisema wakati wa uzinduzi huo ambao ulitangazwa moja kwa moja kwenye vituo vya televisheni nchini humo. Lakini ahadi hii imeibua shutuma kali na kejeli kutoka kwa Wakenya mtandaoni. Takriban wanasiasa 12 tayari wameanza kampeni za kumrithi Rais aliye madarakani Uhuru Kenyatta, ambaye yuko katika miezi ya mwisho ya miaka 10 madarakani.
Picha
kessyngocho.blogspot.  leo October 10/ 2021/nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na za nyuma za Magazeti ya Tanzania

Njoo utazame kilicho andikwa kwa magazeti ya leo nyuma na mbele trh 08/10/2021

Picha
Picha
kessyngocho.blogspot.com Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam leo October 2/ 2021/nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na za nyuma za Magazeti

BREKING NEWS MO DEWJI ATANGAZA KUJIUZULU KATIKA NAFASI HII SIMBA SC

Picha
Mfanyabiashara na muwekezaji wa Simba SC Mo Dewji ambaye anamiliki 49% ya hisa za Simba SC kwa thamani ya Tsh Bilioni 20 leo ametangaza rasmi kujiuzulu nafasi yake uenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ndani ya Simba SC na nafasi yake itachukuliwa na aliyekuwa makamu wake Salim Abdallah (Try Again). “Mmetuunga mkono kwa miaka minne ya uongozi wangu kama Mwenyekiti wa Bodi, kwenye miaka minne tumepata mafanikio makubwa tumeshinda Ligi mara 4 na kufanya vizuri kwenye Champignons League muda umefika kama Mohammed na tumekubaliana mimi nitajiuzulu kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Simba SC naomba sana msifikie kuwa mimi nimeondoka Simba bali bado ni muwekezaji”

Karibu utazame kilicho andikwa kwenye magazeti ya leo trh 27/09/2021 mbele na nyuma kwa siku ya leo.

Picha

NAKUKARIBISHA UTAZAME KILICHO ANDIKWA NYUMA NA MBELE KWENYE MAGAZETI YA LEO TRH 25/09/2021

Picha
kessyngocho.blogspot.com Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam leo September /25/ 2021 nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na za nyuma za Magazeti ya Tanzania.

BUNGE LAJADILI UJERUMANI KULIPA FIDIA MAUAJI YA KIMBARI

Picha
kessyngocho.blogspot.com Bunge nchini Namibia litajadili makubaliano kati ya nchi hiyo na Ujerumani katika hatua ya kulipa fidia ya wahanga wa mauaji ya kimbari yaliyofanyika kipindi cha ukoloni wa kijerumani ambayo bado hayajasainiwa hadi kufikia sasa,Majadiliano ya bunge nchini Namibia kuhusu makubaliano kati ya nchi hizo yanatarajiwa kuanza tena Jumatano mwezi huu. Spika wa Bunge nchini Namibia, David Nahongandja amesema ana matumaini makubwa katika makubaliano hayo na hatua hiyo itapelekea kupigiwa kura siku zijazo kwa kuwa,Kura hiyo ilicheleweshwa baada ya vikao vya bunge kuahirishwa mwezi Juni kutokana na kuongezeka kwa maambukizi ya virusi vya corona. Kwa mujibu wa Nahongandja, wabunge wa upinzani mara kwa mara waliizuia serikali kuwasilisha makubaliano hayo bungeni hapo kwa siku ya jana,na kupelekea zaidi ya watu 300 waliandamana nje ya jengo la bunge kupinga makubaliano yaliyopendekezwa.

MAHAKAMA KUU IMEFUTILIA MBALI KESI YA MBOWE

Picha
kessyngocho.blogspot.com Mahakama Kuu imefutilia mbali kesi ya Mbowe Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya  Dar es  Salaam  imetupilia mbali kesi ya kikatiba ya Mwenyekiti wa CHADEMA,  Freeman Mbowe  aliyokuwa akilalamika kwamba haki zake za kikatiba zilikiukwa wakati wa kumkamata, kumweka kizuizini na hatimaye kumfungulia kesi akikabiliwa na mashtaka ya ugaidi. Mahakama  hiyo ilifikia uamuzi huo mbele ya Jaji John Mgeta baada ya kukubaliana na hoja moja kati ya tatu za  Serikali  ya pingamizi la awali kuwa maombi hayo hayako sawa kisheria kwasababu yanapingana na kifungu  4(5)  na kifungu cha  8(2)  cha sheria ya haki za msingi na utekelezaji wa majukumu sura ya tatu. Kwamba Mbowe ana njia nyingine za kupata hayo anayo walalamikia. Jaji alisema, wakati maombi hayo yameletwa, wakati huo huo kuna mwenendo wa kesi katika Mahakama nyingine ambako Mbowe anashtakiwa kesi ambayo ndiyo msingi wa malalamiko hayo. Jaji Mgeta alisema Mbowe anatakiwa kuwasilisha malalamiko yake katika Mahakama Kuu Ki