Habari za moja kwa moja
Tanzania imepokea ndege nyingine ya masafa ya kati aina ya Bombardier Dash 8- Q 400 kutoka nchini Canada.
Ndege hiyo ilipokewa na Rais Samia Suluhu Hassan aliyewaongoza viongozi mbalimbali na baadhi ya watanzania waliojitokeza katika uwanja wa kimataifa wa Julius Nyerere.
Hiyo ni ndege ya tisa kati ya 11 zinazotarajiwa kununuliwa na serikali kufikia mwaka 2022, ndege nyingine inatarajiwa kuwasili mwezi Oktoba mwaka huu.
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Dkt Leonard Chamuriho ndege iliyopokelewa leo ni ya 5 ya masafa mafupi kununuliwa na Tanzania tangu mchakato wa kufufua Shirika hilo uanze katika kipindi cha miaka 5 iliyopita.
Akizungumza wakati wa kupokea ndege hiyo, Rais wa nchi hiyo, Samia Suluhu alisema mbali na ndege za abiria nchi hiyo inatarajia kununua ndege nyingine moja ya mizigo.
‘Tunanunu ndege hiyo kwa sababu nchi yetu hivi sasa ni miongoni wa wazalishaji wakubwa wa mbogamboga, matunda na maua, tunatarajia ikifika mwaka 2025 mazao hayo yataingizia nchi yetu dola bilioni 2, hivyo suala la kuwa na ndege ya mizigo ni muhimu’, alisema Rais Samia.
Kufuatia kununuliwa kwa ndege hizo, idadi ya watu wanaosafiri kupitia ndege za Shirika la ndege la nchi hiyo (ATCL) imeongezeka kutoka abiria 4,000 hadi 60,000 kwa mwezi na kufanya umiliki wa soko la usafiri wa anga la ndani kuongezeka kutoka asilimia 2.5% hadi 73%.
Mbali na kuongezeka kwa abiria, Safari za kikanda kupitia ndege za Tanzania zimeongezeka kutoka kituo kimoja cha Comoro mpaka 7, huku zikitarajiwa safari za kimataifa kuongezeka zaidi hivi karibuni pale baadhi ya anga za kimataifa zitakapofunguliwa kutokana na hali ya janga la Corona.
Mpaka sasa ndege zilizowasili Tanzania ni tano aina ya Bombardier Q400, ndege mbili za masafa ya kati ya Airbus A220-300 na nyingine mbili kubwa za masafa marefu ambazo ni Boeing 787 Dreamliner.
Maoni
Chapisha Maoni
Karibu kessyngocho.blogspot.com
Tukuhudumie