kessyngocho.blogspot.comINASIKITISHA, MSIBA MZITO ULIOMPATA MILLARD AYO LEO Mwandishi wa Habari wa Ayo TV, Nellyson Grigery amefariki dunia katika ajali ya gari iliyotokea leo Agosti 18, 2021 katika eneo la Kibaha mkoani Pwani. Taarifa ya Kifo cha mwandishi huyo imethibitishwa na mmiliki wa televisheni hiyo ya mtandaoni, Millard Ayo kupitia ukurasa wake wa Instagram. Millard ameandika “Leo imekua siku ngumu sana kwangu na AyoTV Team tumeondokewa na marafiki zetu wawili na mmoja ni mfanyakazi mwenzetu, mpigapicha wa AyoTV Kanda ya Ziwa, Nellyson Grigery.” “Mwingine ni rafiki yetu Mujitaba Yusuf waliekuwa wakisafiri pamoja kutoka Mwanza kuja Dar. Wamepata ajali Kibaha wakiwa watatu tunamshukuru Mungu mtu wa tatu ambaye ni Khamis Abdallah Mwandishi wa AyoTV Kanda ya Ziwa amejeruhiwa na sasa anaendelea vizuri."
Machapisho
Inaonyesha machapisho kuanzia Agosti, 2021
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
kessyngocho.blogspot.comINASIKITISHA, MSIBA MZITO ULIOMPATA MILLARD AYO LEO Mwandishi wa Habari wa Ayo TV, Nellyson Grigery amefariki dunia katika ajali ya gari iliyotokea leo Agosti 18, 2021 katika eneo la Kibaha mkoani Pwani. Taarifa ya Kifo cha mwandishi huyo imethibitishwa na mmiliki wa televisheni hiyo ya mtandaoni, Millard Ayo kupitia ukurasa wake wa Instagram. Millard ameandika “Leo imekua siku ngumu sana kwangu na AyoTV Team tumeondokewa na marafiki zetu wawili na mmoja ni mfanyakazi mwenzetu, mpigapicha wa AyoTV Kanda ya Ziwa, Nellyson Grigery.” “Mwingine ni rafiki yetu Mujitaba Yusuf waliekuwa wakisafiri pamoja kutoka Mwanza kuja Dar. Wamepata ajali Kibaha wakiwa watatu tunamshukuru Mungu mtu wa tatu ambaye ni Khamis Abdallah Mwandishi wa AyoTV Kanda ya Ziwa amejeruhiwa na sasa anaendelea vizuri."
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
kessyngocho.blogspot.com Chanjo ya Ukimwi yaanza kufanyiwa Majaribio Edwin TZA · 24 minutes ago Wakati chanjo ya corona ikiendelea kutolewa katika Mataifa mbalimbali Duniani, chanjo ya Virusi vya UKIMWI (VVU) iliyokuwa inafanyiwa utafiti muda mrefu na Kampuni ya Moderna ya Marekani inatarajiwa kuanza kufanyiwa majaribio kwa Binadamu leo Jumatano . Kampuni hiyo imetengeneza chanjo za aina mbili za UKIMWI ambazo zimefuzu hatua za awali za kimajaribio na hivyo kuanza kutumika kwa binadamu katika awamu ya tatu, chanjo hizo ni mRNA-1644 na mRNA-1644v2-Core ambazo zimeshachunguzwa na kufanyiwa majaribio ya awali na kuonekana salama kabla ya kujaribiwa kwa Binadamu kwa mara ya kwanza. Chanjo hiyo itaanza kutolewa kwa Watu 56 wenye umri wa kati ya miaka 18 hadi 56 na majaribio yanatarajiwa kukamilika Mwaka 2023.
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
kessyngocho.blogspot.com PICHA 10:Mwenge ulivyokabidhiwa DSM, Wakuu wa Wilaya washuhudia Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Amos Makalla leo August 18 amepokea Mwenge wa Uhuru uliowasili Asubuhi ya leo Uwanja wa ndege wa Mwalimu Nyerere ukitokea Mkoa wa Pwani na kuukabidhi kwa Wilaya ya Ilala kwaajili ya kuanza shughuli ya uzinduzi na uwekaji mawe ya msingi kwenye miradi ya miradi ya maendeleo. Akipokea Mwenge huo kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe. Aboubakar Kunenge, RC Makalla amesema kwa siku tano ambazo Mwenge wa Uhuru utakuwa Dar es salaam utapitia miradi ya maendeleo 46 yenye thamani ya Shillingi Billion 105.1. Mwenge wa Uhuru umeanza rasmi kukimbizwa leo Mkoa wa Dar es salaam kwa kuanzia Wilaya ya Ilala Kisha Ubungo, Kinondoni, Kigamboni na Temeke ambapo ifikapo August 23 Mwenge huo utakabidhiwa kwa Mkoa wa Lindi ukienda na kaulimbiu inayolenga kuhimiza Matumizi sahihi ya TEHAMA . . . . . . . . .
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
kessyngocho.blogspot.com Tambo za Dulla Mbabe kuelekea Pambano lake na Twaha Kiduku “Yule sio Bondia” Edwin TZA · 26 minutes ago Ni kutoka kwenye kambi ya Bondia Dulla Mbabe ambaye amefunguka maandalizi ya pambano lake na Bondia Twaha Kiduku ambalo linatarajiwa kufanyika Ijumaa hii katika Ukumbi wa Ubungo Plaza Dar es Salaam. Bondia huyo akizungumza na Ayo TV & Millardayo.com alisema. ..”Nimeshajiandaa muda tu tumalize mzizi wa fitina , kwanza lazima crown ibaki katika mkoa wa Dar halafu ndipo itaenda Pwani Kisarawe”- Dulla Mbabe Bonyeza Play kufahamu alichozungumza Dulla Mbabe kuhusu Pambano lake dhidi ya Twaha Kiduku
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
kessyngocho.blogspot.com Waziri amvaa vikali Askofu Gwajima “Ananivurugia Wizara, majeshi yote akamatwe” (Video+) Edwin TZA · 2 hours ago Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dr. Doroth Gwajima ameliagiza Jeshi la Polisi na Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa ( TAKUKURU) kumkamata na kumhoji Mbunge wa Kawe Askofu Josephat Gwajima ili athibitishe kauli anazozitoa dhidi ya Serikali na Viongozi kuhusu chanjo ya Covid-19. Dr. Gwajima ametoa agizo hilo leo Jumanne Agosti 17, 2021 katika kijiji cha Kyatunge Butiama na kusema Askofu Gwajima amekuwa akitoa taarifa za kupotosha kwa makusudi jambo linaloivuruga Wizara yake na Serikali katika mapambano dhidi ya ugonjwa huo. “Gwajima ni ndugu yangu, ni shemeji yangu kabisa, lakini mimi ni waziri nimekula kiapo cha kutumikia nchi yangu sio kumtumikia shemeji yangu. Mimi ndiye msemaji wa masuala ya afya nchini, nimechoka kuvuruguwa, naagiza Majeshi yote Poli...
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
kessyngocho.blogspot.com Watalii 250 waingia Tanzania “tahadhari imechukuliwa juu ya Uviko-19 Mamia ya Watalii kutoka Israel waendelea kuja nchini kutembelea vivutio mbalimbali vya utalii licha ya changamoto ya Ugonjwa wa UVIKO-19 ambao umeikumba dunia hivi sasa. Kuja kwa watalii hao kunatokana na sio tu Tanzania kubarikiwa kuwa na vivutio vingi vya utalii, bali pia hatua za tahadhari zinachokuliwa na Serikali dhidi ya maambukizi ya virusi vya UVIKO-19. Hatua hizo ambazo zimewejengea imani watalii kuendelea kuja nchini zimetambuliwa na Baraza la Wasafiri na Utalii Duniani (World Travels and Tourism Council-WTTC) ambapo Mwezi Agosti 2020 baraza hilo liliitangaza Tanzania kuwa nchi salama ya kuitembelea. Akizungumza Jijini Arusha, wakati wa hafla ya kuwapokea watalii takribani 100 kutoka Israel na wengine 150 waliokuwa wanaagwa, Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Hemedi Mgaza amesema ujio wa watalii...
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
kessyngocho.blogspot.com Kimbunga ‘Grace’ kupiga Haiti leo Wakati majonzi yakiendelea kuwakumba Watu wa Haiti kufuatia kukumbwa na tetemeko kubwa la ardhi ambalo limesababisha vifo vya Watu 1,297 jana Jumapili, taarifa mpya kutoka Haiti ni kwamba leo usiku kunatarajiwa kuwa na Kimbunga. Kimbunga hicho kilichopachikwa jina Grace kinatarajiwa kuipiga Haiti leo usiku, kikizidisha machungu ya wakaazi wa Nchi hiyo maskini. Majanga haya yametokea wakati Nchi hiyo ikikumbwa na mzozo wa kisiasa kufuatiwa kuuawa kwa Rais wake, Jovenel Moise mwezi uliopita. Waziri Mkuu Ariel Henry ametangaza hali ya dharura ya mwezi mzima na kuwataka Wahaiti kuonesha mshikamano.
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
kessyngocho.blogspot.com Polisi watoa onyo kwa wanaofumania na kupiga “tunawatafuta” (Video+) Jeshi la Polisi kupitia kwa Msemaji wake wa David Misime ametoa onyo kwa wale wanaojichukulia sheria mkononi kwenye matukio mbalimbali ikiwemo lililotokea Kongowe Dar es Salaam la Fumanizi nakupelekea watu kupigwa ambapo amesema watu hao wameshakamatwa pia Jeshi hilo limezungumzia tukio la kijana aliyedaiwa kuiba nakufungwa kwenye pikipiki nakuburuzwa hadi kupoteza maisha. “Jeshi letu la Polisi linaendelea kutoa Elimu mbalimbali kwa jamii lakini leo hii ningependa kuzungumza kwa uhalifu ambao umeanza kuonekana kwa baadhi ya watu kujichukua sheria mikono naomba nivitaje ili Wananchi waache kujichukulia Sheria mikono kwani ni jambo la aibu sana”- Jeshi la Polisi
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
kessyngocho.blogspot.com Live:Mwijaku anamjibu Manara muda huu “Manara akasome kwanza” Edwin TZA · 1 hour ago NI Mwijaku ambae muda huu anazungumza na Vyombo vya Habari kuhusu kauli za Haji Manara alizozitoka Agosti 4, 2021 akishtumu Uongozi wa Simba SC. “Akubali akatae lazima aende kusoma zama zimebadilika kwasasa mpira unahitaji watu waliosoma, timu zetu zinapoelekea kwasasa zinahitaji watu wenye taaluma kwahiyo asitupie lawama kwa Simba “- Mwijaku Ayo TV iko Mubashara muda huu unaweza ukafuatilia mwanzo mwisho anachozungumza muda huu. MASHABIKI WA SIMBA WAMKINGIA KIFUA MO DEWJI “HATUMTAKI ANAYETOBOA MTUMBWI”