Machapisho

Picha
kessyngocho.blogspot.comINASIKITISHA, MSIBA MZITO ULIOMPATA MILLARD AYO LEO Mwandishi wa Habari wa Ayo TV, Nellyson Grigery amefariki dunia katika ajali ya gari iliyotokea leo Agosti 18, 2021 katika eneo la Kibaha mkoani Pwani. Taarifa ya Kifo cha mwandishi huyo imethibitishwa na mmiliki wa televisheni hiyo ya mtandaoni, Millard Ayo kupitia ukurasa wake wa Instagram.  Millard ameandika “Leo imekua siku ngumu sana kwangu na AyoTV Team tumeondokewa na marafiki zetu wawili na mmoja ni mfanyakazi mwenzetu, mpigapicha wa AyoTV Kanda ya Ziwa, Nellyson Grigery.”  “Mwingine ni rafiki yetu Mujitaba Yusuf waliekuwa wakisafiri pamoja kutoka Mwanza kuja Dar. Wamepata ajali Kibaha wakiwa watatu tunamshukuru Mungu mtu wa tatu ambaye ni Khamis Abdallah Mwandishi wa AyoTV Kanda ya Ziwa amejeruhiwa na sasa anaendelea vizuri."
Picha
kessyngocho.blogspot.comINASIKITISHA, MSIBA MZITO ULIOMPATA MILLARD AYO LEO Mwandishi wa Habari wa Ayo TV, Nellyson Grigery amefariki dunia katika ajali ya gari iliyotokea leo Agosti 18, 2021 katika eneo la Kibaha mkoani Pwani. Taarifa ya Kifo cha mwandishi huyo imethibitishwa na mmiliki wa televisheni hiyo ya mtandaoni, Millard Ayo kupitia ukurasa wake wa Instagram.  Millard ameandika “Leo imekua siku ngumu sana kwangu na AyoTV Team tumeondokewa na marafiki zetu wawili na mmoja ni mfanyakazi mwenzetu, mpigapicha wa AyoTV Kanda ya Ziwa, Nellyson Grigery.”  “Mwingine ni rafiki yetu Mujitaba Yusuf waliekuwa wakisafiri pamoja kutoka Mwanza kuja Dar. Wamepata ajali Kibaha wakiwa watatu tunamshukuru Mungu mtu wa tatu ambaye ni Khamis Abdallah Mwandishi wa AyoTV Kanda ya Ziwa amejeruhiwa na sasa anaendelea vizuri."
Picha
kessyngocho.blogspot.com Chanjo ya Ukimwi yaanza kufanyiwa Majaribio Edwin TZA  ·  24 minutes ago Wakati chanjo ya corona ikiendelea kutolewa katika Mataifa mbalimbali Duniani, chanjo ya Virusi vya  UKIMWI  (VVU) iliyokuwa inafanyiwa utafiti muda mrefu na Kampuni ya Moderna ya Marekani inatarajiwa kuanza kufanyiwa majaribio kwa Binadamu leo  Jumatano . Kampuni hiyo imetengeneza chanjo za aina mbili za  UKIMWI  ambazo zimefuzu hatua za awali za kimajaribio na hivyo kuanza kutumika kwa binadamu katika awamu ya tatu, chanjo hizo ni  mRNA-1644 na mRNA-1644v2-Core  ambazo zimeshachunguzwa na kufanyiwa majaribio ya awali na kuonekana salama kabla ya kujaribiwa kwa Binadamu kwa mara ya kwanza. Chanjo hiyo itaanza kutolewa kwa Watu  56 wenye umri wa kati ya miaka  18 hadi 56  na majaribio yanatarajiwa kukamilika Mwaka 2023.
Picha
kessyngocho.blogspot.com PICHA 10:Mwenge ulivyokabidhiwa DSM, Wakuu wa Wilaya washuhudia Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Amos Makalla leo August 18 amepokea Mwenge wa Uhuru uliowasili Asubuhi ya leo Uwanja wa ndege wa  Mwalimu Nyerere  ukitokea Mkoa wa Pwani na kuukabidhi kwa Wilaya ya Ilala kwaajili ya kuanza shughuli ya uzinduzi na uwekaji mawe ya msingi kwenye miradi ya miradi ya maendeleo. Akipokea Mwenge huo kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe. Aboubakar Kunenge,  RC Makalla  amesema kwa siku tano ambazo Mwenge wa Uhuru utakuwa  Dar es salaam  utapitia miradi ya maendeleo 46 yenye thamani ya Shillingi  Billion 105.1. Mwenge wa Uhuru umeanza rasmi kukimbizwa leo Mkoa wa  Dar es salaam  kwa kuanzia Wilaya ya Ilala Kisha  Ubungo, Kinondoni, Kigamboni na Temeke   ambapo ifikapo August 23 Mwenge huo utakabidhiwa kwa Mkoa wa Lindi ukienda na kaulimbiu inayolenga kuhimiza Matumizi sahihi ya  TEHAMA . . . . . . . . .
Picha
kessyngocho.blogspot.com Tambo za Dulla Mbabe kuelekea Pambano lake na Twaha Kiduku “Yule sio Bondia” Edwin TZA  ·  26 minutes ago Ni kutoka kwenye kambi ya Bondia  Dulla Mbabe  ambaye amefunguka maandalizi ya pambano lake na Bondia Twaha Kiduku ambalo linatarajiwa kufanyika  Ijumaa  hii katika Ukumbi wa Ubungo Plaza Dar es Salaam. Bondia huyo akizungumza na Ayo TV & Millardayo.com alisema. ..”Nimeshajiandaa muda tu tumalize mzizi wa fitina , kwanza lazima crown ibaki katika mkoa wa Dar halafu ndipo itaenda Pwani Kisarawe”- Dulla Mbabe Bonyeza Play kufahamu alichozungumza Dulla Mbabe  kuhusu Pambano lake dhidi ya Twaha Kiduku
Picha
kessyngocho.blogspot.com Waziri amvaa vikali Askofu Gwajima “Ananivurugia Wizara, majeshi yote akamatwe” (Video+) Edwin TZA  ·  2 hours ago Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto  Dr. Doroth Gwajima ameliagiza Jeshi la Polisi na Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa  ( TAKUKURU)  kumkamata na kumhoji Mbunge wa Kawe Askofu  Josephat Gwajima  ili athibitishe kauli anazozitoa dhidi ya Serikali na Viongozi kuhusu chanjo ya  Covid-19. Dr. Gwajima ametoa agizo hilo leo Jumanne  Agosti 17, 2021  katika kijiji cha Kyatunge Butiama na kusema  Askofu Gwajima amekuwa akitoa taarifa za kupotosha kwa makusudi jambo linaloivuruga Wizara yake na Serikali katika mapambano dhidi ya ugonjwa huo. “Gwajima ni ndugu yangu, ni shemeji yangu kabisa, lakini mimi ni waziri nimekula kiapo cha kutumikia nchi yangu sio kumtumikia shemeji yangu. Mimi ndiye msemaji wa masuala ya afya nchini, nimechoka kuvuruguwa, naagiza Majeshi yote Poli...
Picha
kessyngocho.blogspot.com Watalii 250 waingia Tanzania “tahadhari imechukuliwa juu ya Uviko-19 Mamia ya Watalii kutoka Israel waendelea kuja nchini kutembelea vivutio mbalimbali vya utalii licha ya changamoto ya Ugonjwa wa UVIKO-19 ambao umeikumba dunia hivi sasa. Kuja kwa watalii hao kunatokana na sio tu Tanzania kubarikiwa kuwa na vivutio vingi vya utalii, bali pia hatua za tahadhari zinachokuliwa na Serikali dhidi ya maambukizi ya virusi vya UVIKO-19. Hatua hizo ambazo zimewejengea imani watalii kuendelea kuja nchini zimetambuliwa na Baraza la Wasafiri na Utalii Duniani (World Travels and Tourism Council-WTTC) ambapo Mwezi Agosti 2020 baraza hilo liliitangaza Tanzania kuwa nchi salama ya kuitembelea. Akizungumza Jijini Arusha, wakati wa hafla ya kuwapokea watalii takribani 100 kutoka Israel na wengine 150 waliokuwa wanaagwa, Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,  Balozi Hemedi Mgaza  amesema ujio wa watalii...