kessyngocho.blogspot.com Kimbunga ‘Grace’ kupiga Haiti leo Wakati majonzi yakiendelea kuwakumba Watu wa Haiti kufuatia kukumbwa na tetemeko kubwa la ardhi ambalo limesababisha vifo vya Watu 1,297 jana Jumapili, taarifa mpya kutoka Haiti ni kwamba leo usiku kunatarajiwa kuwa na Kimbunga. Kimbunga hicho kilichopachikwa jina Grace kinatarajiwa kuipiga Haiti leo usiku, kikizidisha machungu ya wakaazi wa Nchi hiyo maskini. Majanga haya yametokea wakati Nchi hiyo ikikumbwa na mzozo wa kisiasa kufuatiwa kuuawa kwa Rais wake, Jovenel Moise mwezi uliopita. Waziri Mkuu Ariel Henry ametangaza hali ya dharura ya mwezi mzima na kuwataka Wahaiti kuonesha mshikamano.
Machapisho
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
kessyngocho.blogspot.com Polisi watoa onyo kwa wanaofumania na kupiga “tunawatafuta” (Video+) Jeshi la Polisi kupitia kwa Msemaji wake wa David Misime ametoa onyo kwa wale wanaojichukulia sheria mkononi kwenye matukio mbalimbali ikiwemo lililotokea Kongowe Dar es Salaam la Fumanizi nakupelekea watu kupigwa ambapo amesema watu hao wameshakamatwa pia Jeshi hilo limezungumzia tukio la kijana aliyedaiwa kuiba nakufungwa kwenye pikipiki nakuburuzwa hadi kupoteza maisha. “Jeshi letu la Polisi linaendelea kutoa Elimu mbalimbali kwa jamii lakini leo hii ningependa kuzungumza kwa uhalifu ambao umeanza kuonekana kwa baadhi ya watu kujichukua sheria mikono naomba nivitaje ili Wananchi waache kujichukulia Sheria mikono kwani ni jambo la aibu sana”- Jeshi la Polisi
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
kessyngocho.blogspot.com Live:Mwijaku anamjibu Manara muda huu “Manara akasome kwanza” Edwin TZA · 1 hour ago NI Mwijaku ambae muda huu anazungumza na Vyombo vya Habari kuhusu kauli za Haji Manara alizozitoka Agosti 4, 2021 akishtumu Uongozi wa Simba SC. “Akubali akatae lazima aende kusoma zama zimebadilika kwasasa mpira unahitaji watu waliosoma, timu zetu zinapoelekea kwasasa zinahitaji watu wenye taaluma kwahiyo asitupie lawama kwa Simba “- Mwijaku Ayo TV iko Mubashara muda huu unaweza ukafuatilia mwanzo mwisho anachozungumza muda huu. MASHABIKI WA SIMBA WAMKINGIA KIFUA MO DEWJI “HATUMTAKI ANAYETOBOA MTUMBWI”
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
kessyngocho.blogspot.com Picha:DC Nikki wa Pili ajipatia chanjo ya Uviko 19 Ni Mkuu wa wilaya ya Kisarawe Nickson Simon maarufu kama Nikk wa Pili ambae leo Agosti 5, 2021 amezindua rasmi Chanjo ya kujikinga na Ugonjwa wa Covid-19 katika wilaya yake, baada ya uzinduzi huo pia Mkuu wa Wilaya huyo alishiriki kujipatia chanjo hiyo. Baada ya kujipatia chanjo hiyo alisema “ Tunamshukuru Rais Samia na Serikali kwa ujumla pamoja na wadau wote wa afya kwa kufanikisha upatikanaji wa chanjo hii salama kabisa katika nchi yetu. Hii ni hatua muhimu katika kuendeleza mapambano dhidi ya Corona’ – DC Nickson Simon . . MUSUKUMA AWAVAA WANAOSEMA UKICHOMWA CHANJO UNAGEUKA ZOMBIE “NI MANENO YA WAPUMBAVU”