kessyngocho.blogspot.comMAMBO YA MSINGI SANA KUYAJUA ILI UISHI NA WENZIO VIZURI. 1. Epuka hasira za ovyo na kila mtu, kuwa msikivu kabla ya kukimbilia maamuzi (elewa kuwa ukiwa na hasira huwezi kupata suluhu ya jambo) 2. Usiwatendee wengine ubaya ukadhani kuwa utakuwa salama (ubaya hulipwa kwa ubaya, ipo siku ubaya wako kwa wengine utakurejea kama sio kuwarejea watu wa kizazi chako) 3. Usichukue maamuzi kabla ya kutafiti ukweli (pengine wapo wanadamu wanaopenda kuonekana wao wema kwa kuumiza wengine). Mtuhumu mtu lakini mpe muda wa kumsikiliza, usimshambulie mtu kwa maneno makali bila kuujua ukweli, ukijua ukweli nafsi inaweza kukusuta. 4. Mchukulie kila mwanadamu ni mkosaji (tambua kuwa hata wewe unawakosea sana wengine na wanakuvumilia. Hivyo usiwe mwepesi wa kuwaadhibu wenzio kwa ubaya). 5. Usipande mbegu ya chuki na ubaya katika jamii unayoishi ukadhani itakuacha salama (chuki hukua kama mti utambaao, ukiipanda ndani ya jamii yako, haitatoka kwako...