Tanesko

WAZIRI wa Nishati, Medard Kalemani ameonya tabia ya baadhi ya Mameneja wa Shirika la Umeme (TANESCO) kuwauzia nguzo wananchi wanaotaka kuunganishiwa huduma ya umeme wakati nguzo hizo utolewa bure kwa wateja kote nchini.

Akizungumza na Mameneja wa TANESCO wa nchini nzima katika semina iliyofanyika Jijini Dodoma, Waziri Kalemani amesema kumekuwa na malalamiko kutoka kwa wananchi juu ya kuuziwa nguzo licha ya Serikali kutoa maelekezo yakutouzwa kwa nguzo hizo.

“Yapo maeneo watu mnawauzia nguzo, pamoja na kutoa maelekezo chungu nzima wabunge wanalalamika ,wananchi wanalalamika tunatoa maelekezo lakini bado hamsikii, naomba niwahoji nani bado analipisha nguzo huko?” alihoji Kalemani.

Licha ya suala hilo, Waziri huyo ameoonya wale wanaounganisha umeme kwa zaidi ya bei ya Shilingi 27,000 ambayo amesema ndiyo bei halali nje ya Dar es salaam.

Amesema yapo maeneo ambayo bado watu wanaunganishiwa umeme kwa kati ya Shilingi 100,000 na 177,000 jambo ambalo amesema siyo sahihi na kwamba atakayeendelea kufanya hivyo atafukuzwa kazi.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

DARAJANI TANZANITE DAR ESALAAM