Machapisho

WATOTO WAWILI WAFARIKI KWA KUKOSA HEWA

Picha
kessyngocho.blogspot.com Watoto wawili wa familia moja wenye umri wa mwaka mmoja na mwingine wa mmoja na nusu wamefariki dunia baada ya kukosa hewa ya kutosha kwasababu ya uwepo wa jiko la moto ndani ya nyumba waliyokuwa wamelala na wazazi wao kwa lengo la kujikinga na baridi huko katika Kijiji cha Usuhilo Manispaa ya Tabora. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, ACP Richard Abwao amekiri kutokea kwa tukio hilo la kuhuzunisha nyumbani kwa Athuman Shaban huku akiwataja watoto waliofariki kuwa ni Aman Athuman mwaka mmoaja na nusu (1.6) na Zainab Athuman aliyekuwa na mwaka mmoja (1). Chanzo cha kifo hicho ni jiko la moto lililokuwa limewekwa ndani ili kusaidia kujikinga na baridi walipokuwa wamelala ndani na wazazi wao ambapo katika tukio hilo watu watatu bado hali zao siyo nzuri na wamelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tabora Kitete huku watoto wawili waliofariki tayari wameshazikwa huko Kijiji cha Usuhilo.
Picha
kessyngocho.blogspot.com
Picha
kessyngocho.blogspot.com- Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam February 2, 2022,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na za nyuma za Magazeti ya Tanzania.

HABARI ZA MAGAZETI TANZANIA KILA SIKU

Picha
kessyngocho.blogspot.com- Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam January 30, 2022,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na za nyuma za Magazeti ya Tanzania.
Picha
kessyngocho.blogspot.com LIVE: Rais Samia anahutubia Taifa usiku huu Muda huu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan anahutubia Taifa kuelekea miaka 60 ya Uhuru, bonyeza PLAY hapa chini kutazama LIVE
Picha
kessyngocho.blogspot.com Mkurugenzi wa gereza ahukumiwa miaka mitano Mahakama ya Rwanda imemuhukumu kifungo cha miaka mitano jela aliyekuwa Mkurugenzi wa Gereza kuu la Kigali kwa kosa la kuiba pesa za mfungwa wa Uingereza. Innocent Kayumba, ambaye alihukumiwa Ijumaa jioni pamoja na makamu wake wa zamani Eric Ntakirutimana, amekata rufaa dhidi ya hukumu hiyo, hati ya mahakama inaonyesha. Mahakama ilimwachilia mfungwa mtaalamu wa IT ambaye alitumia ujuzi wake kudukua kadi ya Visa ya mwathiriwa baada ya kuiambia mahakama kwamba alilazimishwa na mkurugenzi wa gereza kufanya hivyo. Alisema alitakiwa “kuichambua” kadi iliyohifadhiwa na uongozi wa magereza baada ya kubaini kuwa akaunti ya benki iliyounganishwa nayo ilikuwa na kiasi kikubwa cha fedha. Mfungwa huyo mwenye uraia wa Uingereza na Misri aliiambia mahakama kwamba zaidi ya £7,000 ($9,300) zilichukuliwa kutoka kwa akaunti yake kwa kutumia kadi yake mwaka jana bila yeye kujua. Mahakama ilisema Kayumba na naibu wake walipanga njama ya w...
Picha
kessyngocho.blogspot.com Mikopo kwa watakaofunga ndoa Mgombea urais nchini Kenya ameahidi mikopo ya kati ya $4,400 (£3,300) na $8,800 kwa wanandoa wote wapya iwapo atachaguliwa kuwa Rais katika uchaguzi utakaofanyika mwakani. Gavana wa Machakos Alfred Mutua, ambaye alikuwa akizindua ilani yake ya urais Jumapili, alisema mkopo wa riba ya chini utakaolipwa ndani ya miaka 20 utasaidia familia “kuanza maisha vizuri”. Vilevile mgombea huyo amesema serikali yake itahimiza upandaji miti na kuhesabiwa kama sehemu ya malipo ya mahari. “Unapoenda kulipa mahari, unapaswa kusema umepanda miti mingapi,” Bw. Mutua alisema wakati wa uzinduzi huo ambao ulitangazwa moja kwa moja kwenye vituo vya televisheni nchini humo. Lakini ahadi hii imeibua shutuma kali na kejeli kutoka kwa Wakenya mtandaoni. Takriban wanasiasa 12 tayari wameanza kampeni za kumrithi Rais aliye madarakani Uhuru Kenyatta, ambaye yuko katika miezi ya mwisho ya miaka 10 madarakani.