kessyngocho.blogspot.com MAISHA HAYANA FORMULA LAKINI YANA SIRI NYINGI! CHUKUA HIZI 11, KAMA ZITAKUFAA 1. SIRI YA KWANZA Tengeneza connection na watu usitengeneze urafiki, Iko siku marafiki uliowatengeneza watakugeuza Chakula Cha kula maana "kikulacho kinguoni kwako!", Siyo rahisi rafiki akakubali upate zaidi yake! 2. SIRI YA PILI Usimwamini sana rafiki yako ,kwa sababu huyo rafiki yako ana rafiki yake ambaye Wewe si rafiki yako!, Kama hunielewi subiri siku umseme bosi wako akurekodi halafu amrushie boss wako then boss wako ukurushie. Utatamani kufa 3. .SIRI YA TATU Kuna njia tatu tu za kufanikiwa maishani. Njia hizo ni 1.bahati, 2.kipaji 3.bidii yenye akili!, Jitafute ulipo! Huna bahati, huna kipaji halafu unalala mchana? 4. .SIRI YA NNE: Ukiwa na marafiki watano majambazi tegemea kuwa jambazi wa sita; ukiwa na marafiki watano wahuni tegemea kuwa muhuni wa sita, ukiwa na marafiki watano mabilionea tegemea kuwa bilionea wa sita; kasheshe ni masikini kumpata rafiki bili...
Machapisho
Inaonyesha machapisho kuanzia Februari, 2022
WATOTO WAWILI WAFARIKI KWA KUKOSA HEWA
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
kessyngocho.blogspot.com Watoto wawili wa familia moja wenye umri wa mwaka mmoja na mwingine wa mmoja na nusu wamefariki dunia baada ya kukosa hewa ya kutosha kwasababu ya uwepo wa jiko la moto ndani ya nyumba waliyokuwa wamelala na wazazi wao kwa lengo la kujikinga na baridi huko katika Kijiji cha Usuhilo Manispaa ya Tabora. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, ACP Richard Abwao amekiri kutokea kwa tukio hilo la kuhuzunisha nyumbani kwa Athuman Shaban huku akiwataja watoto waliofariki kuwa ni Aman Athuman mwaka mmoaja na nusu (1.6) na Zainab Athuman aliyekuwa na mwaka mmoja (1). Chanzo cha kifo hicho ni jiko la moto lililokuwa limewekwa ndani ili kusaidia kujikinga na baridi walipokuwa wamelala ndani na wazazi wao ambapo katika tukio hilo watu watatu bado hali zao siyo nzuri na wamelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tabora Kitete huku watoto wawili waliofariki tayari wameshazikwa huko Kijiji cha Usuhilo.