kessyngocho.blogspot.com Kizz Daniel kutotokea kwenye show, Str8upvibes watoa tamko Uongozi wa Str8up Vibes ambao ndiyo Waandaaji wa Tamasha la Summer Amplified wametoa tamko kufuatia Msanii wa Nigeria Kizz Daniel kushindwa kutotokea kabisa ukumbini kutumbuiza usiku wa kuamkia leo kama ilivyotakiwa na kupelekea Mashabiki kukasirika. Taarifa ya Str8up Vibes leo imesema “Sisi katika Str8upVibes tunasikitika sana kwa kilichotokea kwenye Tamasha la SUMMER AMPLIFIED Aug 07 2022 ambapo Kizz Daniel hakutumbuiza kama ilivyotarajiwa, tunakubali kwamba hii imesababisha kuvunjika moyo kwa Wateja wetu waaminifu na Wadau muhimu wa muda mrefu waliohusika, tunachukua hatua zinazofaa katika kushughulikia suala hili kwa ukali na kuuhakikishia Umma na mashabiki waliolipa na kuhudhuria kwamba tunafanya kila tuwezalo kuhakikisha tunaweka hali vizuri, tunaomba subira yao tunaposhughulikia hili” “Str8up Vibes ni kampuni inayoheshimika na iliyojijengea sifa thabiti, kuridhisha Wateja wetu siku zote imekuwa j...