Machapisho

Picha
kessyngocho.blogspot.com Harmonize adaiwa kumtoa Kizz Daniel Polisi, DC aingilia kati ‘Watu Wakiahidiwa wapate fedha zao’ Agosti 8, 2022 Mwimbaji wa Nigeria Kizz Daniel alivyofuatwa hotelini kwake na kuchukuliwa na Polisi Dar es salaam . Saa kadhaa ikaripotiwa kuwa Harmonize alifika kituoni na kumchukua msanii huyo basi julikana taarifa yoyote. Sasa leo Agosti 9, 2022 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Godwin Gondwe ametangaza kuingia kati sakata hilo la msanii wa Nigeria. Stori kamili unaweza ukabonyeza play kufahamu zaidi.
Picha
kessyngocho.blogspot.com Kizz Daniel kutotokea kwenye show, Str8upvibes watoa tamko Uongozi wa Str8up Vibes ambao ndiyo Waandaaji wa Tamasha la Summer Amplified wametoa tamko kufuatia Msanii wa Nigeria Kizz Daniel kushindwa kutotokea kabisa ukumbini kutumbuiza usiku wa kuamkia leo kama ilivyotakiwa na kupelekea Mashabiki kukasirika. Taarifa ya Str8up Vibes leo imesema “Sisi katika Str8upVibes tunasikitika sana kwa kilichotokea kwenye Tamasha la SUMMER AMPLIFIED Aug 07 2022 ambapo Kizz Daniel hakutumbuiza kama ilivyotarajiwa, tunakubali kwamba hii imesababisha kuvunjika moyo kwa Wateja wetu waaminifu na Wadau muhimu wa muda mrefu waliohusika, tunachukua hatua zinazofaa katika kushughulikia suala hili kwa ukali na kuuhakikishia Umma na mashabiki waliolipa na kuhudhuria kwamba tunafanya kila tuwezalo kuhakikisha tunaweka hali vizuri, tunaomba subira yao tunaposhughulikia hili” “Str8up Vibes ni kampuni inayoheshimika na iliyojijengea sifa thabiti, kuridhisha Wateja wetu siku zote imekuwa j
Picha
kessyngocho.blogspot.com Picha: Rais Samia alivyolipokea Kombe la Dunia Ikulu Dar es Salaam Ni Mei 31, 2022 ambapo Rais Samia akipokea Kombe la Dunia la Mashindano ya Mpira Miguu (World CUP) Litakaloshindaniwa nchini Qatar IKulu Dar es Salaam. Hizi ni baadhi ya picha mbalimbali  ushuhudie yaliyojiri Ikulu Dar es Salaam. . . . . . . .

DARAJANI TANZANITE DAR ESALAAM

Picha
kessyngocho.blogspot.com Ni Mei 28, 2022 ambapo watu mbalimbali wamefika katika  Daraja Tanzanite Dar es Salaam  kushuhudia live fainali kati ya Real Madrid na Liverpool kupitia Big Screen iliyofungwa kwenye daraja hilo. Hapa unaweza tazama picha mbalimbali shangwe za mashabiki wa Mpira waliofika kujionee fainali hiyo inayoendelea muda huu. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .
kessyngocho.blogspot.com MAISHA HAYANA FORMULA LAKINI YANA SIRI NYINGI! CHUKUA HIZI 11, KAMA  ZITAKUFAA 1. SIRI YA KWANZA Tengeneza connection na watu usitengeneze urafiki, Iko siku marafiki uliowatengeneza watakugeuza Chakula Cha kula maana "kikulacho kinguoni kwako!",  Siyo rahisi rafiki akakubali upate zaidi yake! 2. SIRI YA PILI Usimwamini sana rafiki yako ,kwa sababu huyo rafiki yako ana rafiki yake ambaye  Wewe si rafiki yako!, Kama hunielewi subiri siku umseme bosi wako akurekodi halafu amrushie boss wako then boss wako ukurushie. Utatamani kufa 3. .SIRI YA TATU Kuna njia tatu tu za kufanikiwa maishani. Njia hizo ni 1.bahati, 2.kipaji 3.bidii yenye akili!, Jitafute ulipo! Huna bahati, huna kipaji halafu unalala mchana? 4. .SIRI YA NNE: Ukiwa na marafiki watano majambazi tegemea kuwa jambazi wa sita; ukiwa na marafiki watano wahuni tegemea kuwa muhuni wa sita, ukiwa na marafiki watano mabilionea tegemea kuwa bilionea wa sita; kasheshe ni masikini kumpata rafiki bilionea

WATOTO WAWILI WAFARIKI KWA KUKOSA HEWA

Picha
kessyngocho.blogspot.com Watoto wawili wa familia moja wenye umri wa mwaka mmoja na mwingine wa mmoja na nusu wamefariki dunia baada ya kukosa hewa ya kutosha kwasababu ya uwepo wa jiko la moto ndani ya nyumba waliyokuwa wamelala na wazazi wao kwa lengo la kujikinga na baridi huko katika Kijiji cha Usuhilo Manispaa ya Tabora. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, ACP Richard Abwao amekiri kutokea kwa tukio hilo la kuhuzunisha nyumbani kwa Athuman Shaban huku akiwataja watoto waliofariki kuwa ni Aman Athuman mwaka mmoaja na nusu (1.6) na Zainab Athuman aliyekuwa na mwaka mmoja (1). Chanzo cha kifo hicho ni jiko la moto lililokuwa limewekwa ndani ili kusaidia kujikinga na baridi walipokuwa wamelala ndani na wazazi wao ambapo katika tukio hilo watu watatu bado hali zao siyo nzuri na wamelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tabora Kitete huku watoto wawili waliofariki tayari wameshazikwa huko Kijiji cha Usuhilo.